
Uchunguzi
uliofanywa na wanahabari katika zoezi la kukusanya kero za sekta binafsi linaondelea
kupitia mitandao ya jamii ya Twitter na Facebook umeonyesha kuwa wakazi wa
jijini Dar es Salaam wanakabiliwa na mgao wa umeme kwa kipindi kirefu sasa.
Hali
hiyo imebainika wakati wa majumuisho ya kero za wateja wa huduma na bidhaa
mbalimbali nchini Tanzania katika
mzunguko wa tatu ambapo Shirika la Ugavi wa Umeme TANESCO limechukua nafasi ya
kwanza kati ya biashara 36 zilizotajwa kuwa kero kwa wateja.
Jumla
ya kero tofauti 220 zimewasilishwa na wateja toka zoezi hilo lianze ambapo
Shirika la Tanesco lina jumla ya kero 71 ambapo kati ya hizo 60 ni kutoka Dar
es Salaam pekee.
Katika
mzunguko huu nafasi ya pili ilishikiliwa
na Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo yenye kero 63 kati ya 220 huku nafasi ya tatu ikiwaendea Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom yenye kura
17 kati ya 220 zilizowasilishwa.
No comments:
Post a Comment