Huku masaa yakizidi kuyoyoma kuelekea muda ambao
msemaji wa klabu ya El Merreikh alioutoa kwa mchezaji Mrisho Ngassa kujitokeza
alikojificha na kufanya taratibu za uhamisho wake kwenda Sudan - mapema asubuhi
ya leo, kuna taarifa za ndani kabisa kwamba mchezaji huyo ameamua rasmi kurudi
kwenye klabu yake ya zamani ya mitaa ya
jangwani.
Chanzo cha habari kilicho karibu na mchezaji husika na
klabu ya Yanga ni kwamba Mrisho Ngassa tayari amekubaliana kimsingi na Yanga
kwamba atajiunga na klabu hiyo baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo
uliobakisha miezi isiyopungua sita na klabu ya Simba kwa malipo mazuri kama ambavyo imekuwa kwa mchezaji Haruna
Niyonzima.
"Ni kweli Ngassa tayari ameshakuwa na pre-contract na
Yanga ya miaka miwili, kwa sasa hivi amepewa millioni 10 na fedha nyingine atapewa mara atakapomaliza mkataba wake na Simba mwishoni mwa msimu.
Sasa hivi mchezaji amejificha ili kuepeuka usumbufu wa El Merreikh na Simba
pamoja na Azam."
Mrisho Ngassa amekuwa
katika vichwa vya habari kwa takribani wiki mbili
sasa juu ya usajili wake wa kwenda kujiunga na El
Merreikh ambao wamemuahidi mshahara wa $4000 kwa mwezi pamoja na $75000 kama ada ya usajili, huku vilabu vyake vya Simba
na Azam FC vikilipwa
$100,000.
No comments:
Post a Comment