Tuesday, December 18, 2012

TAMKO LA BAVICHA MWANZA KUHUSU KUTAKA KUMNNG'OA MADARAKANI DR SLAA.


KAULI YA VIJANA WA CHADEMA MKOA WA MWANZA
KWA nafasi yangu ya Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) Mkoa wa Mwanza, nimelazimika kutoa ufafanuzi na kuweka kumbukumbu sawa na kutuliza munkari ya vijana wa mkoa huu na nchi nzima kutokana na habari zilizosambazwa kwa njia mbalimbali za upashanaji habari.
Imeripotiwa katika njia hizo za upashanaji habari kuwa BAVICHA wanataka Katibu Mkuu wetu wa Chama, Dkt. Willibrod Slaa, aondoke madarakani na kwamba asipoondoka, wataandaa mandamano ya kumng’oa.
Napenda kutumia nafasi hii kusema maneno machache juu ya upuuzi huo ambao kila mtu anajua umetokana, unaratibiwa na kusimamiwa na CCM, ikiwa eti ndiyo moja ya mikakati ya Sekretarieti ya chama hicho inayoitwa kuwa ni mpya.
Kwa nafasi yangu, mimi ndiye msemaji mkuu wa masuala yote yanayohusu BAVICHA kwa mkoa wa Mwanza. Kwa mamlaka yangu ninaelewa fika vijana wa Mwanza hawajawahi, wala hawana mpango wa kubeba propaganda za CCM dhidi ya CHADEMA na viongozi wetu kuanzia ngazi ya chini hadi ya juu, akiwemo Katibu Mkuu, Dkt. Slaa.
Natumia fursa hii kuwaondolea wasiwasi vijana wa CHADEMA mahali kokote ndani na nje ya nchi, vijana wa Mwanza tuko imara kukilinda chama chetu na viongozi wetu dhidi ya propaganda za CCM na serikali ambazo zina lengo ya kudhoofisha harakati za kujenga taasisi imara inayobeba matumaini ya Watanzania kwa ajili ya ukombozi wa awamu ya pili.
Natumia nafasi hii pia kuwataka vijana wa CHADEMA Mkoa wa Mwanza watulie, wakisubiri BAVICHA Mkoa ifanye maamuzi kwa kuzingatia maslahi mapana ya umma wa Watanzania na chama chetu dhidi ya hila, njama na uchu wa mtu mmoja mmoja miongoni mwetu ambaye anaamua ‘kufika bei’ na kubeba propaganda za CCM.
Napenda kuwaambia vijana wa CHADEMA kuwa mapambano ambayo chama chetu kinayaendesha kiasi cha kutishia CCM kuendelea kuwepo madarakani mwaka 2014 na 2015, ni mapambano ya haki dhidi ya udhalimu, ni mapambano ya matumaini dhidi ya kukataa tama, ni mapambano ya uadilifu dhidi ya ufisadi.

Wednesday, December 12, 2012

MAUAJI YA KUTISHA MKOANI MARA,WATU WAKATWA VICHWA,SERIKALI YADAIWA KUTUMIA WAANDISHI FAKE KUKANUSHA UKATILI HUO





Na George Marato,Musoma
Kufuatia mauji ya kinyama na kutisha kuibuka mkoani Mara,hatimaye jeshi la Polisi mkoani humo,limetoa tahadhari kubwa kwa wananchi wa Mkoa huo hasa  Wanawake wa maeneo ya vijijini kuwa makini  wakati wakiwa katika shughuli kilimo na utafutaji wa kuni.
Pamoja na tahadhari hiyo pia wananchi hasa wanawake wameombwa kutoa taarifa polisi pindi tu wanaposhuku kuwepo kwa jambo lolote ambalo linahatarisha maisha yao ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mara SSP Japhet Lusingu,ametoa taadhari hiyo jana ofisi kwake mjini hapa wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na matukio ya mauji ambayo yameibuka katika siku za hivi karibuni mkoani Mara hasa katika wilaya ya Butiama na Manispaa ya Musoma .
Alisema tayari jeshi la polisi linawashikiria watu sita kuhusiana na mauji ya Sabina Mkireri mkazi wa kijiji cha Kiemba ambaye aliuawa kwa kuchinjwa kisha wauji kuondoka na kichwa chake Desemba tatu mwaka huu.
“Nachukua nafasi hii kuwatoa hofu wananchi kuhusu mauji haya,lakini natoa taadhari kwa wakina mama hasa wa maeneo ya vijijini wanapokuwa katika shughuli za kilimo na utafutaji wa kuni wawe waangalifu na watoe taarifa mapema pindi tu wanaposhuku kuwapo kwa jambo lolote lisilo la kawaida”alisema kaimu kamanda huyo ambaye pia ni afisa mnadhimu wa jeshi la polisi mkoa wa Mara.
Aidha alisema Desemba mbili mwaka huu majira ya saa moja usiku Brandina Peru alikutwa polini akiwa amekufa baada ya kuchinjwa.
Kaimu kamanda huyo wa polisi mkoa wa Mara,alisema marehemu kabla ya kuuawa kikatili aliondoka nyumbani kwake desemba mosi mwaka huu akiwa peke yake kwenda porini kukata kuni na hakuweza kurudi nyumbani hadi alipokutwa amekufa kwa kuchinjwa.
Hata hivyo alisema kabla ya kuchinjwa wauaji hao walimvua nguo zote na kuweka kando kisha kumbaka na kwamba hakuna mtu yoyote aliyekamatwa hadi sasa na chanzo cha tukio bado kinachunguzwa.
Kwa sababu hiyo alisema jeshi la polisi limejipanga kikamilifu kwaajili ya kuwasaka watu wanahusika na vitendo hivyo huku akiwaamba waandishi wa habari na viongozi wa kisiasa kutowatia hofu wananchi kwa kutoa taarifa bila kuthibitishwa na vyombo vya dola.
Kuhusu taarifa za viungo hivyo vya binadamu kutumika kwa imani potofu kwa shughuli za uchimbaji wa madini na uvuvi wa samaki alisema jeshi hilo linachunguza ukweli wa taarifa hizo.
Wakati huo huo,kamanda Lusingu,alisema mwanafunzi mmoja Hamis Lazaro wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya Etaro ameuawa kwa kushambuliwa,mawe na kukatwakatwa na mapanga katika sehemu mbalimbali za mwili wake.
Alisema tukio hilo lilitokea saa 11.30 katika kijiji cha Kwikerege kata ya Etaro wilaya Butiama baada ya kukutwa chini ya uvungu wa kitanda kilichokuwa kikitumiwa na Nyakongo Nyangata ambaye alikuwa na mahusiano ya kimapenzi.
Hata hivyo kamanda huyo alisema mbali na madai ya marehemu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi huyo mwenzake lakini wananchi walijichukulia sheria mkononi baada ya kuisi kuwa ni miongoni mwa watu ambao wamekuwa wakishiriki katika vitendo vya mauji ya kinyama katika eneo hilo.
Mwisho
Na George Marato,Musoma
SAKATA la mauji ya kinyama mkoani Mara,imani za kishirikina ni moja ya sababu kubwa ambazo zimetajwa kuwa chanzo kikuu cha mauji hayo ambayo yameibuka kwa kasi  kubwa katika mkoa huu hasa kwa wilaya za Butiama na Musoma mjini huku wauaji wakichukua baadhi ya viungo vya binadamu kwa madai ya kusadia shughuli za uvuvi wa samaki na uchimbaji wa dhahabu.
Imedaiwa kuwa wauji hao wengi wamekuwa wakitoka mkoa wa Kigoma wakiwa ni wenyeji wa nchi jirani ya Congo ambao wamekuwa wakishirikiana na wenyeji katika maeneo hayo kisha kufanya mipango ya mauji hayo ya kinyama.
Baadhi ya wavuvi na wachimbaji wadogo wa madini,wamedai kuwa wauji hao wamekuwa wakiuza vichwa vya watu kwa imani za kishirikina kwaajili ya shughuli za uchimbaji wa dhahabu huku ndimi,matiti na sehemu za siri vikitumika kwaajili ya uvuvi katika ziwa Victoria.
Aidha imedaiwa kuwa baadhi ya Mangariba pia kutoka eneo la Tarime na Kiagata wamekuwa wakiwauzia wavuvi viungo vya mwanamke baada ya kuwakeketa jambo ambalo limetajwa kuwa chazo cha kusababisha wimbi la mauji ya watoto wa kike ambao wamekuwa wakiuawa kisha kunyofolewa viungo hivyo yakiwemo na matiti.
Hata hivyo baadhi ya wavuvi ambao wameomba kuhifadhiwa majina yao kutoka visiwa ndani ya ziwa victoria wakizungumza kwa njia ya simu na Nipashe Jumapili kwa nyakati tofauti,wamedai kuwa pamoja na matajiri wao kununua viungo hivyo kutoka kwa baadhi ya watu lakini hakuna mabadiliko yoyote ambayo wamekuwa wakiyapata.
“Kweli kuna wakati watu wanakuja eti ni waganga kisha wanakwenda ziwani usiku na matajiri na mwakilishi wa wavuvi kwa kila mtumbwi ili  kuonyesha nyavu zilipo wakifika wanachukua vitu kama nyama wanasugua kila mwesho wa nyavu lakini hatujawahi kuona mabadiliko ya kuongeza samaki”alisema mmoja ya wavuvi.
Wavuvi hao waliongeza kuwa watu hao wanaoisi kuwa ni waganga wamekuwa wakiwazuia kuongea kitu chochote wakati wa zoezi la kufanya mitambiko hiyo huku wao wakizungumza lugha na maneno wasio yaelewa hadi zoezi hilo linapo malizika.
Walipohojiwa ni kwanini wanashindwa kutoa taarifa hizo kwa vyombo vya dola wavuvi hao walidai kuwa wanashindwa kufanya hivyo kwa kuhofia maisha yao kwa vile wamiliki wengi wa zana hizo za uvuvi wana mahusiano makubwa na baadhi ya maafisa ambao wako katika vyombo vya dola.
Hata hivyo wachimbaji hao wa dhahabu wameshindwa kuwa wazi kila walipoulizwa ili kuthibitisha viungo hasa vichwa vya binadam vimekuwa vikitumika wakati gani na kwa maeneo yapi.
Kwa upande wake mbunge wa Musoma vijijini Nimrod Mkono,pamoja na kutoa pole kwa wote ambao wamekumbwa na janga hilo,lakini alisema jeshi la polisi linapaswa kuwachunguza wanasiasa kwani alisema wakati mwingine wamekuwa wakishiriki katika ushirikina huo kwaajili ya kujipatia fedha.
“Hali hii inatisha inawezekana vitu hivi vikatumika kwa ushirikina katika madini na uvuvi lakini miongoni mwetu wanasiasa ni vyema tukachunguzwa kwani wengini hawamuogopi mungu wanaweza kufanya mchezo huo mchafu kwaajili ya kupatafuta pesa za uchaguzi na wengine kufanyia mitambiko ya biashara zao”alisema Mkono kwa njia ya simu na kuongeza
“Hilo ni jambo kubwa haiwezekani mtu wa kawaida tu akaenda kumchinja mtu na kuondoka na kichwa chake bila ya kuwapo kwa mkono wa watu wenye uwezo,hivyo ni vyema jeshi la polisi likafanya uchunguzi wa kina kuhusu hali hii”alisema.
Juzi mbunge Musoma mjini Vicent Nyerere(Chadema) alimtaka mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP)Said Mwema kuchukua hatua sasa kuhusu mauji mauji ya kikatili ambavyo yameibuka katika Manispaa ya Musoma na wilaya ya Butiama.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu alisema katika kipindi cha mwezi mmoja tu zaidi ya watu kumi na saba wameuawa huku wengine wakichinjwa kicha waujia kuondoka na vichwa na viungo vyao vingine vya miili yao.
Alisema pamoja na hali hiyo ambayo imechangia hofu kubwa kwa wananchi lakini hakuna jitihada zozote zinazochukuwa kwaajili ya kukabiliana na vitendo hivyo vya kinyama.
Aidha mbunge huyo alimtaka pia Rais Jakaya Kikwete kuchukua hatua kwa wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama wa wilaya hizo ambao amedai baadhi yao wameshindwa kusimamia majukumu yao na kubaki kuendesha siasa wakati wananchi wakizidi kuawa kinyama na wengine kuachwa na vilema vya maisha.
“Ni tatizo kubwa ndani ya mwezi mmoja tu watu kumi na saba wameuawa kinyama na wengine kuchinjwa lakini mbali na vyombo vya dola kukaa kimya hata nyinyi waandishi mmeshindwa kujulisha umma kuhusu ukatili huu”alisema Nyerere na kuongeza.
“Rais mtoe mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya(DC) hapo Musoma amekalia siasa na kuacha majukumui ya serikali katika kulinda raia na mali zao hii ni hatari kubwa”aliongeza.
Hata hivyo wakati mbunge huyo akitoa kauli hiyo,mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Butiama Angelina Mabula,ameliagiza jeshi la polisi kufanya kazi usiku na mchana katika kuhakikisha linawatia mbaloni watu wote ambao wanahusika na mauji ya kikatili ya raia.
Mabula ambaye ni mkuu wa wilaya ya Butiama,alitoa agizo hilo juzi jioni baada ya kuokotwa kwa mama mmoja Sabina Mkereri (46)ambaye alichinjwa na wauji kuondoka na kichwa chake katika kijiji cha Kabegi kata kata ya Nyakatende.
“Nawaomba wananchi mtoe ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha wahusika wote wanasakwa na kuanzia sasa naagiza kuanza kwa vikundi vya ulinzi shirikishi kwaajili ya kufanya kazi ya kuwasaka watu hawa usiku na mchana…jamani tunaipeleka wapi Tanzania yetu yenye amani kwa kufanya matendo haya ya kinyama”alisema DC Mabula.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mara SSP Japhet Lusingu,akizungumza na gazeti hili pamoja na kukiri baadhi ya watu kuchinjwa na viungo vyao kuchukuliwa lakini alisema idadi inayotajwa si sahihi.
Alisema tayari jeshi la polisi limechukua hatua mbalimbali za kukabiliana na vitendo hivyo vya kinyama huku akisema jeshi lake linachunguza kuhusu viungo hivyo kutumika kwa shughuli za uvuvi na ushirikiana.
Hata hivyo aliwaomba waandishi na viongozi wa siasa kuacha kutoa taarifa ambazo si sahihi bila kuthibitishwa na jeshi hilo ili kutowaweka katika hali ya hofu wananchi.

MRISHO NGASA ACHA UTOTO

Huku masaa yakizidi kuyoyoma kuelekea muda ambao msemaji wa klabu ya El Merreikh alioutoa kwa mchezaji Mrisho Ngassa kujitokeza alikojificha na kufanya taratibu za uhamisho wake kwenda Sudan - mapema asubuhi ya leo, kuna taarifa za ndani kabisa kwamba mchezaji huyo ameamua rasmi kurudi kwenye klabu yake ya zamani ya mitaa ya jangwani.

Chanzo cha habari kilicho karibu na mchezaji husika na klabu ya Yanga ni kwamba Mrisho Ngassa tayari amekubaliana kimsingi na Yanga kwamba atajiunga na klabu hiyo baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo uliobakisha miezi isiyopungua sita na klabu ya Simba kwa malipo mazuri kama ambavyo imekuwa kwa mchezaji Haruna Niyonzima.

"Ni kweli Ngassa tayari ameshakuwa na pre-contract na Yanga ya miaka miwili, kwa sasa hivi amepewa millioni 10 na fedha nyingine atapewa mara atakapomaliza mkataba wake na Simba mwishoni mwa msimu. Sasa hivi mchezaji amejificha ili kuepeuka usumbufu wa El Merreikh na Simba pamoja na Azam."

Mrisho Ngassa amekuwa katika vichwa vya habari kwa takribani wiki mbili sasa juu ya usajili wake wa kwenda kujiunga na El Merreikh ambao wamemuahidi mshahara wa $4000 kwa mwezi pamoja na $75000 kama ada ya usajili, huku vilabu vyake vya Simba na Azam FC vikilipwa $100,000.

MADAKTARI WALIOMFANYIA UPASUAJI TYSON WANENA


Mike Tyson 'Michelle' ambaye anayedaiwa kujibadili na kuwa mwanamke.


BINGWA mashuhuri wa zamani wa uzito wa juu duniani, Mike Tyson, anasemekana yuko katika hali nzuri baada ya kujibadili na kuwa mwanamke katika operesheni aliyofanyiwa huko Beverly Hills, Marekani, hivi karibuni ambapo amebadili jina na anajiita Michelle.
Kuna wakati Tyson alikuwa anajulikana kama “Mtu mwenye sura mbaya zaidi duniani”!

Tyson ambaye amebadili jina na kujiita Michelle.

“Watu wanaona ni ajabu mie kuwa mwanamke hivi sasa,” alisema Tyson ambaye aliwahi kufungwa kwa kubaka, na ambaye amefanyiwa mabadilko kadhaa ya uso, pua na viungo vingine kwa masaa 16. Aliongeza kwamba: “Hata nilipokuwa bondia nilikuwa natamani sana kuwa na matiti na nyeti za mwanamke.”

Iron Mike au Iron Maiden kama anavyojulikana sasa aliyasema hayo akiwa ametulia huku amevaa wigi la kike, suruali ya ‘jeans’ ya bluu na T-shirt yenye picha ya Vanessa Bruno ambapo alidokeza kwamba mara sehemu zote nyeti za kike zitakapojitokeza atawadhihirishia Wamarekani kwamba yeye si “mvulana mbaya” tena.
Amesema ameutunza uume wake ulioondolewa katika chupa ili kuwakumbusha wabaya wake waliokuwa wakimfanyia vitendo vya kuchukiza yeye na “wavulana wazuri” wengine huko gerezani.
Japokuwa wachambuzi wa masuala ya ndondi mwanzoni walishangazwa na maneno hayo ya Tyson, wengi wamekiri kwamba alama za yeye kupenda hivyo zilikuwepo.

Mmoja amesema kwamba: “Huko nyuma, alikuwa anapenda sana kuvaa sana glovu za kike, viatu virefu vya ngozi vya kike na magauni ya hariri, na pia alikuwa ni mtu mwenye kupenda sana heleni.”

MAMA KANUMBA AMBARIKI MRITHI WA MWANAYE



MAMA wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa ametoa baraka zake kwa mwigizaji chipukizi, Philemon Lutwaza ‘Uncle D’ ambaye anatarajia kuigiza katika filamu ya After Death ambayo ni maalum kwa kumuenzi marehemu mwanaye, Imelda Mtema anashuka nayo.
Akizungumza na paparazi wetu juzikati, mama Kanumba ameweka plain kuwa ameridhishwa na uwezo wa Uncle D na anaimani kuwa ataweza kuziba pengo la marehemu katika nafasi ya kucheza na watoto wale aliokuwa akiigiza nao marehemu
Namshukuru sana Jacqueline Wolper kwa kuandaa filamu ya After Death maalum kwa ajili ya kumuenzi mwanangu. Nina imani kila kitu kitakwenda vizuri na mimi nimewapa baraka zote ,” alisema mama huyo.

Tuesday, December 11, 2012

BONDIA MIKE TYSON KUBADILI JINSIA NA KUWA MWANAMKE



Mike Tyson
NEW YORK, Marekani
BINGWA wa zamani wa ndondi uzito wa juu, Mike Tyson anadaiwa kubadilisha jinsia kutoka kuwa hali ya kiume na kuwa kike.

Habari za kufanyiwa upasuaji huyo kwenye hospitali moja mjini, Beverley Hills, Marekani ziliteka mitandao kadhaa ya kijamii, huku pia gazeti la The Standard likiwa na habari hiyo.
Hata hivyo, habari hizo hazijathibitishwa ramsi ingawa mpaka jana jioni mitandano mingi ya kijamii ilikuwa na taarifa hizo.

Bingwa huyo wa zamani aliyejitaja kama �Mwanaume mbaya duniani�, mzaliwa wa Brooklyn, aliwaambia waandishi wa habari kuwa siku kwanza atakayopata hedhi (kuona siku zake) ndiyo itakuwa kamilisho la ndoto yake.

Lakipi pia katika kuhakikisha anakamilisha dhamira yake ya kuwa mwanamke, amesema kuanzia muda huo jina lake ramsi sasa litakuwa Michelle.

"Baadhi ya watu wanaweza kudhani mimi ni mtu wa ajabu kwa sababu sasa ni mwanamke," alisema bingwa huyo wa zamani wa ndondi aliyewahu kuhukumiwa kwa shitaka la kubaka.

Upasuaji wa kubadilisha jinsia ya Tyson ulichukua takribani masaa 16, akibadilishwa sura, rangi na mambo mengine ya kumfanya avutie kama mwanamke.

�Pamoja na ubabe wangu ulionifanya kuwa mpiganaji mzuri, sikuwahi kupoteza hali yangu ya uanamke na nilijua ipo siku moja matiti yataota na pia nitakuwa na sehemu za siri za mwanamke.

Tyson, maarufu kama 'Iron Mike au Iron Maiden', aliyewahi kumng'ata meno bondia, Evander Holyfield walipodundana mwaka 1996, alipandikizwa homoni za kike zitakazomfanya kuwa na tabia za jinsia hiyo.

Tyson, akiwa amevalia wigi, suruali aina jeans yenye nyeusi na fulana ya rangi ya Bluu na kuonekana mwenye furaha, alisema kubadilishwa kwake viungo na kuwekwa vya kike, kunathibitisha mwisho wa tabia yake mbaya.

Pamoja na watangazaji wa ndondi kushangazwa na hatua hiyo ya Tyson, lakini wengi wamekubali kwamba kuna mabadiliko ya kitabia yameonekana. "Amabadilisha kimavazi, mwonekano na kizuri zaidi amekuwa mpole," taarifa zilidai.
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa mbalimbali za uzushi zikiwahusu watu maarufu, ambapo katika ya mwaka huu msanii Eddie Murphie alidaiwa kufa katika ajali ya boti ya kuteleza kwenye barafu.

Msanii mwingine aliyehushishwa na uzushi huo ni Will Smith ambaye naye alikumbwa na kadhia ya kudaia kufa. Wote wako hai mpaka sasa.

SHEREHE YA MIAKA 7 YA THT ILIVYOFANA DAR LIVE


Familia ya THT ikiwa jukwaani wakati wa kusherehekea miaka 7 toka kuanzishwa.
Shilole na kundi lake wakilishambulia jukwaa la Dar Live.
Vijana wa THT wakiwasha moto wakati wa sherehe yao ya kutimiza miaka 7 ndani ya Dar Live usiku wa kuamkia leo.
Msanii Ben Pol akiwajibika stejini.
Shilole akimdatisha shabiki aliyepanda stejini.
Shetta akiwapa raha mashabiki.
Dogo Aslay akiwadatisha mashabiki.
Ommy Dimpoz akiimba na mashabiki waliofurika ndani ya Dar Live.
Mwanadada Sundi Gaga kutoka THT akionyesha swagga zake jukwaani.
Dancer wa THT akionyesha machejo jukwaani.
Nyomi iliyohudhuria sherehe hizo.
Wapenzi wa burudani wakifurahia shangwe wakati wa sherehe hizo.
Mzee Yusuf na vijana wake wakipagawisha stejini.
DJ Bulla kutoka Clouds FM akifanya vitu vyake.
Queen Darleen akiwarusha mashabiki.
Msanii Godzilla akiwapa raha mashabiki wake.
Dogo Aslay na Bi. Cheka wakikamua.
Diva Loveness wa Clouds FM akiwasabahi mashabiki.
...Burudani zikiwa zimepamba moto.
Rachel akiwapagawisha mashabiki wake.
Juma Mataluma akifanya mambo.
...Mpaka chini.
Shangwe zikizidi kukolea ndani ya Dar Live.
Ben Pol akicheza na mashabiki wake.
Msanii Ditto akiwapa tano mashabiki.
Linah akiwa stejini.
--
WASANII wa nyumba ya vipaji, Tanzania House of Tallent ‘THT’ usiku wa kuamkia leo waliangusha bonge la pati ndani ya Ukumbi wa Dar live uliopo Mabagala jijini Dar kusherehekea miaka 7 ya kuanzishwa kundi hilo la kukuza vipaji. Katika pati hiyo wasanii mbalimbali wa muziki walitoa burudani hasa wasanii wenyewe wa THT. Pichani juu ni baadhi ya matukio yaliyojili ukumbini hapo.