![]()
Chadema
wakiwa katika maandamano.
---
Madiwani hao ni Estomih Mallah (aliyekuwa Naibu Meya ya
Manispaa ya Arusha kipindi hicho), John Bayo aliyekuwa Diwani wa Elerai, Reuben
Ngowi (Themi), Charles Mpanda (Kaloleni) na Rehema Mohamed aliyekuwa Diwani wa
Viti Maalumu.
--
Na Mussa
Juma
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, imewaamuru
madiwani watano waliotimuliwa Chadema kulipa gharama za kesi waliyokuwa
wamefungua kupinga kufukuzwa uanachama, vinginevyo watapelekwa magereza.Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Charles Magesa alitoa hukumu hiyo jana baada ya
Chadema kushinda kesi hiyo.
Hakimu Magesa alisema madiwani hao wanapaswa kulipa
Sh15 milioni ndani ya miezi miwili, wakishindwa watapelekwa
gerezani.
Madiwani hao ni Estomih Mallah (aliyekuwa Naibu Meya ya
Manispaa ya Arusha kipindi hicho), John Bayo aliyekuwa Diwani wa Elerai, Reuben
Ngowi (Themi), Charles Mpanda (Kaloleni) na Rehema Mohamed aliyekuwa Diwani wa
Viti Maalumu.
Pia, katika kesi hiyo ya madai Chadema walikuwa
wakiwakilishwa na Wakili Method Kimomogoro, wakati wadaiwa hao walikuwa
wakijitetea wenyewe baada ya aliyekuwa wakili wao kujitoa.
Akisoma uamuzi huo, Hakimu Magesa alisema baada ya
mahakama kupitia hoja za pande zote, imeona wadaiwa hao wanapaswa kulipa zaidi
ya Sh15.1 milioni, kila mmoja anatakiwa kulipa zaidi ya Sh3.2 milioni katika
kipindi kisichozidi miezi miwili.
Awali, kulikuwa na mvutano kati ya wadaiwa
hao jambo lililosababisha kesi hiyo kusikilizwa kwa kipindi kirefu ambapo
walitakiwa kueleza mahakama hiyo sababu ya kutokupelekwa gerezani, huku kila
mmoja akitamka kiwango cha fedha ambacho angeweza kulipa kwa
mwezi.
Kwa upande wake, Ngowi alisema ana uwezo wa
kulipa Sh25,000 kwa mwezi, Mpanda Sh20,000, Mallah Sh20,000, Rehema Sh15,000 na
Bayo Sh15,000 kwa mwezi bila kuonyesha mchanganuo wa kipato chao, jambo
lililopingwa vikali na Wakili Kimomogoro kwamba kiwango hicho ni
kidogo.
Hakimu Magesa alisema kisheria mtu akishinda
kesi ana uwezo wa kuchagua hukumu ya kulipwa kwa kuchukua mali za mdaiwa au
mlalamikiwa kupelekwa kifungoni.
“Kimsingi mtu anaposhinda kesi lazima alipwe
gharama aliyotumia na iwapo mahakama itaridhia alipwe kwa kiwango hicho,
itachukua muda mrefu kati ya miaka 10 na 16 kumaliza deni hilo, jambo
litakalosababisha aliyeshinda kushindwa kuona matunda ya ushindi wake,” alisema
Magesa.
Alisema
fedha hizo wanapaswa kuzilipa mara mbili,awamu ya kwanza inatakiwa kila mmoja
kulipa zaidi ya Sh1.5 milioni na wawe wamemaliza kwa miezi miwili na kwamba,
iwapo watashindwa mdai anaweza kupeleka mchanganuo wa gharama za kumtunza
mfungwa na mahakama kuupitia na baadaye kutoa amri wapelekwe
gerezani.
|
|
Thursday, November 22, 2012
KESI YA MADIWANI WA CHADEMA WALIOFUKUZWA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment