
Mwimbaji chipukizi
wa Nyimbo za Injili, George Haule, amipakua Albam yake ya kwanza inayokwenda kwa
jina la Mwamba ni Yesu na sasa ipo mtaani.
Akizungumza na
Father Kidevu Blog, mtumishi huyo wa Mungu amesema albam yake ina nyimbo 8
lakini Mwamba ni Yesu ndio uliyobeba jina la albam yake hiyo ya
kwanza.
Haule amewaomba
watanzania na wapenzi wa nyimbo za injili nchini kumuunga mkono katika harakati
zake hizo za kumuimbia Mungu.
Amezitaja nyimbo
zilizomo katika labam yake hiyo kuwa ni Mwamba ni Yesu uliyobena jina la albam,
Watakiri Mungu Mkubwa, Gusa Maisha Yangu, Nimeona Wala sijasimuliwa, Nadunda
Mugati Mwa Yesu, Longa na Yesy, Tunapendeza na Safari na
Yesu.
Haule amesema Albam
hiyo ni kazi nzuri iliyofanywa na Waandaaji watatu wa muziki wa Injili,
Edwad/Laulence Nguno na Muba Tach.
Amesema albam yake
hiyo inasambazwa na Kampuni ya Usambazaji ya Umoja Audio Visual EA Limited au
GMC kwa Mamu, na yeyote anaetaka kazi hiyo afike kwa wasambazaji
hao.
Haule anatoa
shukrani zake za wachungaji, viongozi na wa umini wote wa BCIC, Temeke kwa
maombi yao pamoja na wote walio pokea ujumbe wa albam yake na wakabarikiwa na
wakaniombea.
Haule namalizia kwa
kusema “Mungu hawezi kumuacha Mwanadamu anae mtii amina.”
Kwa Mawasiliano
zaidi ni
+255 752644040 au +255
802405
Barua pepe: ghaule@rocketmail.com
No comments:
Post a Comment