Msanii wa Kikundi cha
ngoma za asili cha Bujora akiwaburudisha wakazi wa Mwanza katika kucheza na
nyoka aina ya chatu katika uzinduzi wa Kampeni ya Wazazi
nipendeni.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Khalid Mohamed ‘TID’
al-maarufu Mnyama akiwaburudisha wakaazi wa jiji la Mwanza waliofika kwenye
viwanja vya nyamagana kushuhudia uzinduzi wa Kampeni hii ya wazazi
nipendeni!
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist
Ndikilo akipata maelezo kutoka kwa afisa wa shirika la Agakhan, pale
alipotembelea banda lao katika maadhimisho ya uzinduzi wa kampeni za Wazazi
Nipendeni. Hospitali ya Agakhan ilikuwa ni baadhi ya wadau walioshiriki katika
sherehe hizi na kutoa bure huduma za kiafya kwa wajawazito wa jiji la Mwanza.
Sherehe hizi ziliandaliwa na kampuni ya Footprint ya Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment